Home Habari za michezo KISA SARE YA JANA KAGERA….YANGA ‘WALIFELIA’ KWENYE ‘ENGO’ HII HAPA….

KISA SARE YA JANA KAGERA….YANGA ‘WALIFELIA’ KWENYE ‘ENGO’ HII HAPA….

Habari za Yanga leo

Dakika 90 za mchezo wa kagera Sugar dhidi ya Yanga zilimalizika na wageni kulazimishwa sare isiyo na mabao na kushindwa kuwashusha vinara wa Ligi Azam FC.

Mchezo huo uliopigwa Uwanja wa CCM Kaitaba Yanga imeshindwa kupata bao lolote ikiwa ni sare ya kwanza msimu huu kwenye mechi zao 12 ilizocheza.

Yanga imeangushwa na kukosa ubunifu wa kuipangua ngome ya Kagera ambao muda mwingi wa mchezo wamekuwa wakicheza nyuma ya mpira wakitumia mbinu za kujilinda na kuwanyima utulivu wageni wao kufika kirahisi langoni kwao.

Mabingwa hao watetezi hawakuwa na kasi kama ambayo ilikuwa ikionyesha kwenye mechi 11 zilizopita ambapo Kagera waliwafungia njia za kirahisi za kukamilisha mashambulizi yao.

Licha ya kumtumia mshgambuliaji wao mpya Joseph Gueye aliyeingia kipindi cha pili dakika 56 sambamba na mshambuliaji Mzambia Kennedy Musonda bado Yanga ilikosa mbinu za kubadilisha ubao wa mabao.

Matokeo hayo yanaifanya Yanga kusalia nafasi ya pili ikifikisha alama 31 sawa na zile za vinara Azam lakini matajiri hao wa Chamazi wakibaki juu kwa tofauti nzuri ya mabao ya kufunga na kufungwa ingawa wana mchezo mmoja zaidi ya Yanga.

SOMA NA HII  FT:YANGA 2-2 AZAM FC....'FEI TOTO' AFANYA MAAJABU YA DUNIA...MAYELE AFANYIWA 'UNDAVA'...MORRISON MHHH...