Home Uncategorized ISHU YA YAKUB MOHAMED KUIBUKIA SIMBA IMEFIKIA HAPA

ISHU YA YAKUB MOHAMED KUIBUKIA SIMBA IMEFIKIA HAPA


UONGOZI wa Azam FC umesema kuwa kwa sasa bado ina mkataba na nyota wao Yakub Mohamed ambaye inaelezwa kuwa saini yake inawindwa na Simba.

Beki huyo raia wa Ghana ni miongoni mwa wachezaji wenye uhakika wa namba kikosi cha kwanza kutokana na ubora wake.

Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abdulkarim Amin amesema kuwa bado Yakub ni mali ya Azam kwa sasa hivyo ikiwa kuna timu ambazo zinaiwinda saini yake ni lazima zifuate utaratibu.

“Yakub ana mkataba mrefu ndani ya Azam FC kwa sasa hivyo ikiwa kuna timu ambazo zinahitaji saini yake natambua kwamba zinatambua utaratibu ulivyo na namna ya kufanya ili kupata saini za wachezaji wetu,” .

Yakub kandarasi yake ndani ya Azam FC ni ya muda wa miaka miwili ambapo aliongeza mkataba huo msimu uliopita akiwa na mkataba wa mwaka mmoja mkononi ambao unameguka mwishoni mwa msimu huu hivyo ataanza kuishi ndani ya mkataba mpya alioongeza msimu uliopita.

SOMA NA HII  NAMUNGO KAMILI GADO KUVAA MBEYA CITY LEO SOKOINE