Home Uncategorized CORONA YATIBUA MECHI YA ASEANL NA MANCHESTER CITY

CORONA YATIBUA MECHI YA ASEANL NA MANCHESTER CITY


MCHEZO wa Ligi Kuu England kati ya Manchester City dhidi ya Arsenal uliopaswa uchezwe leo Jumatano kwenye Uwanja wa Etihad, umeahirishwa kutokana na bosi wa timu ya Olympiacos na Notingham Forest, Evangelos Marinakis kugundulika na virusi vya Corona.


Bosi huyo inaripotiwa kuwa alionana na watu wa Arsenal siku 13 zilizopita na imebainika kwamba ana virusi hivyo jambo ambalo limewafanya FA kuamua kuahirisha mchezo huo huku ukichukuliwa uamuzi wa watu aliokutana nao kuchukuliwa vipimo.

Ushauri huo umetokana na bosi huyo kuambiwa kwamba anapaswa afuate maelekezo na wale ambao aliweza kuonanana nao hivi karibuni wanapaswa wakae nyumbani kwa muda wa siku 14 na wafanyiwe vipimo pia.


Wachezaji wa Aresanl ambao walikuwa wanajiandaa na mchezo huo wamepewa ruhusu ya kubaki nyumbani kwa muda wa siku 14 na wale ambao walikutana na bosi huyo watakaa nyumbani pia kwa siku 14.


Uongozi wa Arsenal umesema kuwa unamuombea bosi huyo arejee kwenye ubora wake huku wachezaji wengine ambao wapo salama wataanza mazoezi Ijumaa kujiaandaa na mchezo wao dhidi ya Brighton.

SOMA NA HII  SIMBA YAIPA KASI YANGA SASA KESHO KUMALIZANA NA KMC