Home Simba SC MKATA UMEME WA SIMBA LWANGA APEWA KAZI MAALUMU

MKATA UMEME WA SIMBA LWANGA APEWA KAZI MAALUMU

 


MKATA umeme chaguo la kwanza la Kocha Mkuu wa Simba, Didier Gomes, Thadeo Lwanga imebainika kwamba aliwekwa akiba kwa ajili ya mechi ya robo fainali kwa kuhofia kwamba huenda jembe hilo lingeonyeshwa kadi ya njano.

Lwanga ambaye anaaminika kukata umeme kwenye mechi kubwa za kimataifa pamoja na zile za Ligi Kuu Bara, ana ana kadi mbili za njano jambo lililofanya machale ya Gomes yawake mapema kwa kutomuanzisha kabisa.

Nyota huyo raia wa Uganda kwenye mechi za Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi Simba ikiwa imecheza jumla ya mechi sita amecheza mechi tano na kutumia jumla ya dakika 430.

Mchezo wake wa kwanza chini ya Gomes ilikuwa dhidi ya AS Vita ugenini na kwa kukata kwake umeme kulisababisha aonyeshwe kadi moja ya njano na timu yake haikuruhusu bao ila ilishinda kwa bao 1-0.

Mechi ya pili ilikuwa mbele ya Al Ahly Uwanja wa Mkapa na Simba ilishinda bao 1-0, wa tatu ulikuwa mbele ya Al Merrikh ugenini Simba haikuruhusu bao alionyeshwa kadi moja ya njano na ule wa nne ilikuwa mbele ya Al Merrikh, Simba ilishinda mabao 3-0 Uwanja wa Mkapa.

Mchezo wa tano ilikuwa mbele ya AS Vita wakati wakitinga hatua ya robo fainali kwa ushindi wa mabao 4-1, katika mechi ambazo Lwanga alianza Simba haikupoteza mchezo na ilifungwa bao moja pekee katika dakika 450 alikosekana kwenye mchezo dhidi ya Al Ahly wakati Simba ikipoteza mchezo wake wa kwanza kwa kufungwa bao 1-0.

Hivi karibuni Lwanga alisema kuwa huwa hachezi rafu ila anatimiza majukumu yake uwanjani.

Gomes amesema kuwa hakumpanga kwenye mchezo dhidi ya Al Ahly kwa sababu maalumu.

SOMA NA HII  HAJI MANARA: TUNAIFUNGA YANGA NA UBINGWA TUNACHUKUA