Home Uncategorized NAHODHA TANZANITE: KICHAPO KINAWAHUSU WAPINZANI WETU KESHO

NAHODHA TANZANITE: KICHAPO KINAWAHUSU WAPINZANI WETU KESHO

ENEKIA Kasonga, nahodha wa timu ya Taifa ya Wanawake ya Tanzania chini ya miaka 20, amesema kuwa kesho wanaendeleza moto wao wa ushindi kwenye michuano ya COSAFA.

Tanzanite wamealikwa kwenye michuano hiyo inayofanyika nchini Afrika Kusini na mchezo wa kwanza jana ilishinda kwa mabao 2-0 dhidi ya Botswana.

Kesho watashuka uwanjani kumenyana na Eswatini mchezo wao wa pili utakaochezwa Uwanja wa Gelvaland.

“Morari kwa wachezaji kwa sasa ni kubwa hasa baada ya kushinda mchezo wa kwanza tuna amini tutafanya vizuri na tupo tayari kwa ushindani,” amesema.

SOMA NA HII  KOCHA MPYA SIMBA ATOA MAAGIZO HAYA KWA MASTAA KABLA HAJATUA NCHINI