Home Azam FC AZAM WAIPELEKA YANGA KWA MKAPA….BODI YA LIGI WATIA BARAKA…

AZAM WAIPELEKA YANGA KWA MKAPA….BODI YA LIGI WATIA BARAKA…

Uwanja wa Mkapa

UONGOZI wa Azam FC umethibitisha kukubaliwa ombi lao na Serikali kuutumia uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es Salaam kama uwanja wa nyumbani katika michezo yao miwili ya Ligi Kuu Tanzania Bara wanapocheza na Yanga na Simba.

Ofisa habari wa Azam FC, Zakaria Thabit ‘Zaka’, amesema walipeleka barua ya maombi serikalini kwa ajili ya kuomba kutumi uwanja wa Mkapa katika michezo yetu mikubwa miwili ya Simba na Yanga.

Amesema wamefanikiwa na juzi wamepokea majibu kutoka kwa Serikali kuwa wanaruhusiwa kutumia uwanja huo kama wa nyumbani katika michezo hiyo na wataanza dhidi ya Yanga.

“Kikubwa tumekubaliwa kutumia uwanja wa Benjamin Mkapa, tutaanza kutumia uwanja huo katika mechi yetu ijayo dhidi ya Yanga, Machi 16, mwaka huu pamoja na Simba ambao tutacheza nao mzunguko wa pili.

Kikosi chetu chini ya Kocha Youssouph Dabo anaendelea kuwajenga wachezaji kimbinu na kiufundi, kisaikolojia kuhakikisha tunafanikiwa kutumia uwanja huo vizuri na kuvuna pointi muhimu katika michezo hiyo miwili,” alisema Zaka.

Ameongeza kuwa kikosi kipo kambini kinaendele na maandalizi ya mchezo huo kuhakikisha wanafanya vizuri na kufikia katika malengo yao ya sasa kutafuta alama muhimu katika kila mechi.

Zaka amesema lengo lao kubwa ni kutafuta pointi tatu na kuona timu yao inafikia malengo yao kwa sababu wanaangalia zaidi mikakati yao na hawataingia katika katika vita vya mbio za ubingwa wa ligi kuu.

SOMA NA HII  MSHERY 'KUPIGWA KISU' TUNISIA...YANGA WAAMUA LIWALO NA LIWE...ISHU NZIMA IKO HIVI...