Home Habari za michezo KIUNGO MKENYA ATUA BONGO KIMYA KIMYA…AIFUATA SIMBA AKIWA NA BARUA YA WASAUZI…DILI...

KIUNGO MKENYA ATUA BONGO KIMYA KIMYA…AIFUATA SIMBA AKIWA NA BARUA YA WASAUZI…DILI LIKIFELI ANASEPA….


Winga wa kimataifa Mkenya Harrison Mwendwa amewasili nchini asubuhi ya leo akitokea mapumzikoni nchini kwao baada ya Ligi ya Zambia kumalizika akicheza katika klabu ya Kabwe Warrios.

Inaelezwa Mwendwa amewasili hapa nchini kwa ajili ya kufanya mazungumzo ya kimkataba na Simba iliyoonyesha nia ya kumuhitaji tangu dirisha dogo la msimu huu mwezi Januari.

Taarifa inaeleza kama Mwendwa atakubaliana na Simba katika mazungumzo hayo atasaini mkataba wa kuitumikia timu hiyo na kama mambo hayatakwenda vizuri atafanya maamuzi mengine kwani kuna timu zinamuhitaji hapa nchini na Afrika Kusini.

Winga huyo anayetumia mguu wa kushoto aliwahi kutamba na timu za Mathare United, Kariobangi Sharks na AFC Leopards amekuwa akiwindwa na Simba tangu kwenye dirisha dogo la usajil la msimu huu .

SOMA NA HII  KISA MECHI YA SIMBA vs MTIBWA KUSOGEZWA MBELE....'MCHAMBUZI' ATOKWA NA 'POVU' LA MWAKA...