Home Yanga SC YANGA KUMALIZANA NA KIPA HUYU WA BURUNDI

YANGA KUMALIZANA NA KIPA HUYU WA BURUNDI


 YANGA imepania kufanya kweli katika usajili msimu huu, hiyo ni baada ya kukamilisha usajili wa Shabani Djuma, sasa klabu hiyo ipo katika mazungumzo ya mwisho na kipa wa Aigle Noir ya nchini Burundi, Erick Johola.

 

Johola, licha ya kucheza katika Ligi Kuu ya Burundi, lakini ni Mtanzania ambapo kipa huyo alidaka katika mchezo wa kilele cha Wiki ya Mwananchi msimu uliopita na katika mchezo huo licha ya kuonyesha kiwango kikubwa, Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 2-0.

 

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Yanga, Injinia Hersi Said, aliweka wazi kuwa nchini Burundi katika Klabu ya Aigle Noir, wametengeneza urafiki mzuri sana kwa kuingia makubaliano ya baadhi ya mambo, hivyo watu wasishangae kuona wanasajili mchezaji kutoka katika klabu hiyo ambaye tayari walishamfanyia skauti na wamevutiwa naye.

 

β€œBurundi tumetengeneza urafiki mzuri na Klabu ya Aigle Noir na tumekubaliana katika ushirikiano wa baadhi ya mambo na tumevutiwa na mchezaji mmoja, kwa hiyo msishangae kuona kuwa tumesajili mchezaji kutoka hapo.

 

“Tumefanya skauti ya kutosha nchini Burundi, kama ambavyo mnafahamu ni nchi jirani na baada ya mchezo wetu dhidi yao tulikubaliana kushirikiana katika mambo ya maendeleo ambayo ni pamoja na haya ya usajili,” alisema kiongozi huyo.

 

Akizungumza na Championi Ijumaa, Johola alikubali kuwa yupo katika mazungumzo na uongozi wa Yanga ambao unahitaji huduma yake huku yeye akiweka wazi kuwa yupo tayari kujiunga na Yanga iwapo watafikia katika makubaliano mazuri.

 

β€œNi kweli nipo katika mazungumzo na uongozi wa Yanga, wao wameonyesha kuhitaji saini yangu ili niweze kuitumikia, hivyo ndivyo ninavyoweza kukuambia na kama mazungumzo yetu ambayo bado hajakamilika yatafanikiwa kukamilika, basi nitakuwa tayari kujiunga na Yanga,” alisema kipa huyo.


Leo Julai 19 dirisha la usajili limefunguliwa na linatarajiwa kufungwa Agosti 31.

SOMA NA HII  WAKATI WAARABU WAKITAJWA KUMTAKA MAYELE....BOSI YANGA AONYESHA JEURI YA PESA...