Home Yanga SC WAZIRI Jr AIONYESHA YANGA JEURI YA PESA…AWAMWAGIA MAMILION KUVUNJA MKATABA TU

WAZIRI Jr AIONYESHA YANGA JEURI YA PESA…AWAMWAGIA MAMILION KUVUNJA MKATABA TU


STRAIKA Waziri Junior ameiingizia klabu ya Yanga Sh15 milioni baada ya kuvunja mkataba na klabu hiyo kwa kufikia makubaliano ya pande mbili.

Junior alitakiwa kuuzwa kwenda katika klabu ya Dodoma Jiji, lakini mchezaji aliamua kuununua mkataba wake na kumalizana na Yanga moja kwa moja.

Agosti 19 alipewa barua kuonyesha kuwa ni mchezaji huru na anaweza kujiunga na timu ambayo anaitaka mwenyewe.

Kupitia katika ukurasa wake wa Instagram, mchezaji huyo amewaaga mashabiki wa Yanga na kuwatakia kila la heri katika msimu ujao wa Ligi Kuu huku akiwa hajaweka wazi wapi ataibukia.

Junior alisema msimu uliopita haukuwa mzuri kwake licha ya kucheza kwa muda mfupi, lakini malengo yake yalikuwa kufanya vizuri wakati anajiunga na timu hiyo.

“Changamoto ni kawaida kwetu sisi wanamichezo na nimefanya uamuzi mgumu sana, lakini ni lazima nitafute changamoto nyingine kwa ajili ya masilahi ya kipaji changu,” aliandika Junior.

Mchezaji huyo alisajiliwa Yanga msimu wa juzi akitokea Mbao FC alipoifungia timu hiyo mabao 13 na kuchukua tuzo ya mchezaji bora wa mwezi mara mbili, lakini msimu uliopita akiwa na Yanga aliifungia mabao mawili kwenye ligi.

SOMA NA HII  WAKATI SAKHO AKIZIDI KUKIWASHA SIMBA...NKANE APATA 'PANCHA' YANGA...UONGOZI WAJA NA HOJA HIZI...