Home Uncategorized BEKI YANGA AKUBALI MUZIKI WA BEKI YA SIMBA

BEKI YANGA AKUBALI MUZIKI WA BEKI YA SIMBA

 


BEKI wa kati wa Yanga, Lamine Moro raia wa Ghana, ameshindwa kujizuia na kutamka waziwazi kuwa Simba msimu huu wana beki nzuri.

 

Moro ambaye amejiunga na Yanga msimu uliopita akitokea Buildcon FC ya Zambia, msimu huu mpaka sasa amecheza mechi tatu na kufunga mabao mawili kwenye ligi.


Safu ya ulinzi ya Simba inaundwa na Pascal Wawa, Kennedy Juma, Joash Onyango, Ibrahim Ame, David Kameta, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Gadiel Michael na Erasto Nyoni.


Kwa upande wa walinzi wa Yanga msimu huu ni Moro, Bakari Mwamnyeto, Yassin Mustapha, Abdallah Shaibu ‘Ninja’, Said Juma Makapu, Kibwana Shomary, Adeyum Saleh na Paul Godfrey.

 

Moro amesema pamoja na kuwa kikosi chao ni kizuri lakini safu ya ulinzi ya Simba ina ubora mkubwa msimu huu kuliko timu zingine ligi kuu.

 

“Mimi sipendi uongo, mabeki wote wa timu ya Simba wako vizuri hata kama sio timu yangu ila nasema ukweli kuwa Simba wana mabeki wazuri na wenye viwango vya juu,” amesema Moro.



Chanzo:Championi

SOMA NA HII  BENCHI KUMUONDOA KIPA SIMBA