Home Habari za michezo RAIS SAMIA ‘ATIA MKONO’ UWANJA WA YANGA JANGWANI….BENKI YA DUNIA KUMWAGA MABILIONI…

RAIS SAMIA ‘ATIA MKONO’ UWANJA WA YANGA JANGWANI….BENKI YA DUNIA KUMWAGA MABILIONI…

Habari za Yanga leo

Naibu wa Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo, Hamisi Mwinjuma ‘Mwana FA’ amezindua jengo la klabu ya Yanga lililopo Mitaa ya Twiga na Jangwani, jijini Dar es Salaam na kusema Rais Samia Hassan amekubali Benki ya Dunia kuanza mchakato wa ukarabati wa Mto Msimbazi kutakapopatikana eneo la uwanja wa klabu hiyo.

Naibu waziri amesema ilichokifanya Yanga ni jambo kubwa na uongozi chini ya Rais Hersi Said umefanya kazi kubwa na yenye thamani kwani amekuwa akipita nje ya jengo hilo bila ya kudhani kuna shughuli kubwa inafanyika na kuwasifu kwa kuendeleza nguvu zilizoachwa na wazee wao kwa kudumisha jengo hilo.

“Niwapongeze kwa kufikiria na kuweka kwenye utekelezaji wazo la kukarabati na kuanza kulitumia jengo hili upya.”

Mwana FA amesema ana imani wanachama wanaona yanayofanywa na viongozi kutokana na juhudi za Gharib Said Mohamed, mfadhili mkuu wa klabu hiyo na amekuwa na moyo wa kuisaidia klabu hiyo na kuwataka kuendelea kuwahudumia wanayanga kwani viongozi hao ndio walioshikilia furaha yao.

Amesema Rais Samia amekubali mradi wa Benki ya Dunia ufanyike ambao ni marekebisho ya Mto Msimbazi utakaoruhusu klabu hiyo kupata eneo lake itakapojenga uwanja wake kama ilivyo katika mikakati yao.

Aidha alieleza mipango wa serikali juu ya kuboresha mji na kujenga ramani kubwa unaweza kuwa karibu kabisa na jengo hilo ambalo ni faida kwa upande wa Yanga.

“Rais Samia Hassan amekubali Benki ya Dunia juu ya mradi wao wa kuurekebisha Mto Msimbazi. Utaruhusu kuwafidia waliokuwa wanakaa eneo hilo na Yanga kujenga uwanja huo kutokana na ramani ya kuvutia iliyoandaliwa. Kutakuwa na mji unaopendeza na wapenzi wa yanga watajenga uwanja wao na wazo lao hilo limekuja wakati mwafaka.”

Rais wa Yanga Eng Hersi Saidi amesema uzinduzi wa jengo hili ni heshima kwa Rais wa Kwanza wa Zanzibar, Sheikh Abeid Aman Karume ambaye ndiye aliyetoa pesa ya kujenga jengo hili na viongozi wengine waliokuwa sehemu ya uongozi na walioshiriki kujenga jengo hilo.

Jengo hilo ambalo limekarabatiwa na uongozi wa Hersi, limekuwa na sura mpya zikiwamo ofisi ili kukusanya wafanyakazi wote sehemu moja na limegawanyika sehemu mbili.

Amesema sehemu ya kwanza ni sehemu ya chini yenye ofisi zinazohusu utendaji, huku ghorofa ya kwanza na ya pili zikiwa ni vyumba kwa ajili ya wachezaji ‘hosteli’ na ujenzi wa kwanza uliofanyika 1971 ulikidhi vigezo vya jengo linalobeba mahitaji ya timu ya soka na kuwapongeza waasisi wa jengo hilo.

Katika eneo la chini ziliko ofisi za watendaji wa klabu hiyo, yapo mambo mbalimbali na picha zinazobeba kumbukumbu za klabu hiyo, sehemu maalumu ya makombe iliyobeba, kuta zikipambwa na wadhamini na ukumbi wa mikutano kwa ajili ya kuongea na waandishi wa habari na matukio mengine.

Ametaja sababu za kukarabati jengo hilo ni kuenzi kazi kubwa zilizofanya na viongozi waliopita na waliotangulia mbele za haki na hayo ni mafanikio makubwa na itaendelea kujitegemea ili kujinasua katika utegemezi baada ya kuwa katika ofisi za Salamander za GSM kwa miaka mitatu.

Pia amesema sababu nyingine ni watendaji kuwa sehemu moja ili kuhakikisha ufanisi unafanyika na kuruhusu nafasi za wanachama na wapenzi wao kuwafikia viongozi na watendaji wao kwa ukaribu na milango iko wazi kwa wanachama, mashabiki kuja kuhudumiwa kwa ubora unaostahili ikiwamo ishu zinazohusiana na klabu, matawi na hiyo ni ofisi kwa ajili yao.

“Suala lolote la wanachama basi wasisite kufika Kwani watapewa huduma zote wanazostahili tena Kwa wakati bila kusahau Kila kitu kilichorekebishwa kimefanywa na wahandisi wazawa.”

SOMA NA HII  YANGA WAANZA VISIGIZIO MAPEMA

1 COMMENT

  1. Ni ujinga tu unaoendelea hii nchi inauzwa taratibu tu naiona tanzania inaelekea mikononi mwa wazungu rais acha ubaguzi kwanini usitengenezwe uwanja wa simba ambayo mnapata mamilion kupitia yenyewe inawakilisha nchi lakini bado mmeitupa alafu mnakula hela zake acheni ujinga pia acheni ubaguzi huo wote ni ujinga tu?