Home Habari za michezo YANGA WAANZA VISIGIZIO MAPEMA

YANGA WAANZA VISIGIZIO MAPEMA

Habari za Yanga

Klabu ya Young Africans haijafanya mazoezi yake tangu ilipofika nchini Algeria baada ya vifaa vyao kubaki kwenye ndege waliyokuwa wanasafiria.

Mjumbe wa kamati Alex Ngai amesema vifaa hivyo viliwasili baadae pamoja na wachezaji waliokuwa kwenye majukumu ya timu ya Taifa.

“Niwe muwazi tu Kuna changamoto kubwa imetokea ambayo haipaswi kutokea kwa timu ya mpira, mizigo yetu yote ambayo tulikuja nayo ilibaki kwenye ndege jambo ambalo limetupa usumbufu mkubwa. Hatujafanya mazoezi toka tumekuja huku maana mizigo baadhi ilikuja na baadhi ya wachezaji waliowasili Jana waliokuja baada ya mchezo wa Taifa Stars”.

“Licha ya hivyo ila sisi hatujatoka mchezoni, tumeshakuwa wazoefu wa mashindano haya na michezo ya ugenini kwa hivyo sisi tutapambana kesho tupate matokeo”.

SOMA NA HII  SALIM ALLY AISHIKA PABAYA SIMBA..... ISHU IKO HIVI