Home Habari za michezo LICHA YA KIPIGO MALENGO YA TAIFA STARS YAKO PALEPALE KOMBE LA DUNIA

LICHA YA KIPIGO MALENGO YA TAIFA STARS YAKO PALEPALE KOMBE LA DUNIA

Taifa Stars

Morocco moja kati ya timu bora kabisa Afrika kwa sasa ikiwa inashika nafasi ya 13 kwa ubora duniani huku Tanzania kidunia inashika nafasi ya 121. Mchezo wa jana kufuzu kombe la dunia ulikuwa ni mechi nzuri ambayo ilivutia kuitazama.

Moja kati ya vitu vilivyoinyima ushindi ni quality/Ubora wa wachezaji kwa timu zote mbili, Tanzania wachezaji wengi wana quality ya kawaida ambayo wengi ndiyo wanapata uzoefu wa mechi hizi kubwa.

Wachezaji kama Morice Abdallah, Kawawa, Haji Mnoga, Charles, Lusajo Mwaikenda wote hawa ni miongoni wa wachezaji vijana wanaofanya vizuri ila quality yao kulinganisha na wachezaji wengi wa Morocco ni tofauti kabisa.

Morocco ina wachezaji wengi ambao wana uzoefu na mechi kubwa ambapo wamefuzu mara 6 kwenye kombe la dunia, na mara ya mwisho walifika nusu fainali na kuondoshwa na Ufaransa huko Qatar 2022, wachezaji wengi wanacheza soka la kulipwa ulaya kama vile Hakim Ziyech, Achraf Hakimi, Mazroui nk hivyo ushindi wa bao 0-2 walistahili.

Kocha wa Taifa Stars Adel Amrouch inaonesha matumaini makubwa haswa inavyocheza na ikiwa tayari imefuzu kushiriki AFCON ya mwakani huko Ivory Coast, kitendo cha kuwaamini vijana wenye uchu wa mafanikio ni silaha tosha zaidi kwa kocha mkuu kwani kila mchezaji anakuwa na hamu ya kuonesha uwezo wake na kupambana kwa dakika zote.

Kuwa moja wa mastaa wakubwa na matajiri wa kufikia ndoto zako kama wachezaji wa Tanzania na Morocco.

Ile kadi nyekundu ya Mirosho Novatus dhidi ya Soufyane Amrabat ni ya kujitakia ni kweli damu zilichemka lakini Novatus alipaswa kuwa mpole kwakuwa anajua tayari ana kadi moja ya njano.

Kadi hiyo nyekundu huenda ikawa ni pigo kubwa sana kwa kocha na taifa stars kwa sababu itamfanya akose mechi tatu za mashindano, na mechi zote ni muhimu kwa Stars.

SOMA NA HII  MAMBO YAZIDI KUWA MAGUMU KWA KELVIN JOHN NDANI YA KRC GENK...