Home Uncategorized REAL MADRID,CHELSEA ZAKUTANA KWA KIUNGO KAI

REAL MADRID,CHELSEA ZAKUTANA KWA KIUNGO KAI


KAI Havertz, kiungo mshambuliaji wa Klabu ya Bayer Leverkusen anatajwa kuwindwa na Klabu ya Real Madrid iliyo chini ya Kocha Mkuu, Zinadine Zidane.

Inaelezwa kuwa Madrid itapata ushindani mkubwa kutoka kwa Chelsea iliyo chini ya Kocha Mkuu, Frank Lampard ambaye naye pia anatajwa kuiwinda saini ya nyota huyo.

Lampard bado anafikiria kumpata Timo Werner kutoka RB Leipzig jambo hilo linampa matumaini ya kupata saini ya nyota huyo Havertz ili kuunganisha pacha mpya msimu ujao.

Sababu kubwa ya kiungo huyo mwenye miaka 21 saini yake kuwaniwa ni pamoja na uwezo wake wa kucheza akiwa winga pamoja na kujua kufunga mabao jambo linalofanya timu zote mbili kuwa tayari kupata saini yake kwa mujibu wa The Sun.

SOMA NA HII  BALEKE HUYOOO JANGWANI, ISHU KAMILI IKO HIVI YANGA WANABALAA