Home news NYOTA WATANO WA YANGA KUIKOSA KAGERA SUGAR PALE KAITABA

NYOTA WATANO WA YANGA KUIKOSA KAGERA SUGAR PALE KAITABA


KESHO nyota watano wa Yanga wanatarajia kuukosa mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Kagera Sugar ambao ni wa ligi. 

Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nasredddine Nabi kesho ina kibarua cha kusaka ushindi mbele ya Kagera Sugar ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Bara.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Kaitaba, Kagera na utakuwa mubashara ndani ya Azam TV.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Kitengo cha Habari ndani ya Yanga, Hassan Bumbuli ameweka wazi kuwa wapo nyota ambao wataukosa huo mchezo kutokana na sababu mbalimbali.

Miongoni mwa nyota hao ni pamoja na kuhusu wachezaji ambao wamebaki ni Said Ntibanzokiza,’Saido’ ambaye alikosekana pia kwenye mchezo dhidi ya Simba ule wa Ngao ya Jamii.

Yupo beki Yassin Mustapha ambaye amepewa program maalumu kwa ajili ya kurejea kwenye ubora wake baada ya kuwa nje kwa muda akitibu majeraha yake.

 Mukoko Tonombe huyu anatumikia adhabu ya kadi nyekundu aliipata kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho mbele ya Simba, Uwanja wa Lake Tanganyika pia yupo Mapinduzi Balama ambaye naye bado hajawa fiti.

Nyota mwingine ni Dickson Ambundo ambaye aliumia kwenye mazoezi wakati wa maandalizi ya mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Simba.


SOMA NA HII  MFUMO BONASI ZA WACHEZAJI SIMBA WAPANGULIWA....MASTAA AKULIPWA MIL 100 KWA MECHI 5..