Home Uncategorized SABABU ZA UWANJA WA AZAM COMPLEX KUWA SAWA NA TP MAZEMBE HIZI...

SABABU ZA UWANJA WA AZAM COMPLEX KUWA SAWA NA TP MAZEMBE HIZI HAPA


UONGOZI wa Azam FC umesema kuwa tayari ukarabati wa Uwanja wa Azam Complex umekamilika asilimia zote ukiwa sawa na ule wa TP Mazembe huku ukitaja sababu za kuwa sawa na ule wa TP Mazembe kwa ubora.
Ofisa Habari wa Azam FC, Zaka Zakazi amesema kuwa ubora wa uwanja huo kwa sasa ni wa kimataifa.
“Uwanja wetu ubora wake upo sawa na ule Uwanja wa TP Mazembe ya Congo kwa sababu nyasi zake ni 3G, yaani Third Generation ya Artificial (toleo la tatu) turf hii ndio latest version ya Artificial turf, 4G bado ila ule wa zamani ulikuwa ni 2G, kama wa Uhuru, Kaitaba, Karume na Simba
“Hata muundo wa magoli pia ni wa kisasa tofauti na magoli yale ya zamani yaani hapa ni burudani tu mchezaji anaweza kujigonga asihisi maumivu makubwa kwani magoli sio ya chuma ni ya kisasa kabisa, kinachosubiriwa ni shughuli za michezo kurejea mambo yaanze,” amesema.
Kwa sasa Ligi Kuu Bara imesimamishwa kutokana na maambukizi ya Virusi vya Corona na wakati ukifanyiwa marekebisho Azam FC walikuwa wanatumia Uwanja wa Uhuru na Taifa kwa mechi zao za nyumbani.
SOMA NA HII  TANZIA: MJUMBE KAMATI YA UTENDAJI YANGA AFARIKI