Home kimataifa NI VIKOSI GHALI KINOMA ULAYA

NI VIKOSI GHALI KINOMA ULAYA


 UTAFITI ambao umefanywa kwenye timu 98 ambazo zinashiriki zile ligi tano zinazotajwa kufuatiliwa kwa ukaribu zimeweza kuibuka na vikosi ghali kutokana na matumizi ambayo yametumika kwa timu hizo.

Mpaka kufikia Oktoba Mosi 2021 thamani ya vikosi kwa ujumla ipo namna hii kwa upande wa Premier League, Ligue 1, Bundesliga, La Liga na Serie A.

Kwa upande wa Ligue 1 ni kikosi cha PSG ambacho kinatajwa kuwa na thamani kubwa kushinda vyote jambo ambalo linafanya kiwe kwa sasa ni namba moja.

Thamani yake inatajwa kuwa pauni milioni 688 hata kile kikosi kilichoambulia kichapo cha kufungwa mabao 2-1 thamani yake inatajwa kuwa ilikuwa ni milioni 447.

Gharama kubwa ipo kwa nyota wao Kylian Mbappe ambaye ni pauni milioni 120 na thamani ya kikosi hicho inatajwa kuwa kubwa kuliko vikosi 13 vya Ligue 1.


Kwa upande wa Premier ni Manchester United na Manchester City zinatajwa kuwa na vikosi ghali zikiwa zimevuka zaidi ya pauni bilioni moja kutokana na thamani ya vikosi vyao.

Pia Klabu ya Chelsea nao wanaonekana kuwa juu lakini kinara wao anatajwa kuwa City chini ya Pep Guardiola.

Kwa upande wa Bundesliga ni Bayern Munich inatajwa kuwa na thamani kubwa ikiwa inagharimu thamani ya pauni milioni 890 kisha wanafuatiwa kwa mbali na Dortmund ambao thamani yao inatajwa kuwa ni pauni milioni 687.

Ikumbukwe kwamba Bayern Munich kwa sasa wanasaka taji la Bundesliga la 10 mfululizo hivyo lazima moto wao na mkwanja wao uwe juu kinoma.

La Liga ni Barcelona licha ya kwamba kwa msimu wa 2021/21 uwanjani ni majanga matupu kwa kuwa hawana mwendo mzuri.

Licha ya kuondokewa na mastaa wake wakubwa ikiwa ni pamoja na Lionel Messi, ina wachezaji ambao thamani yake ni pauni milioni 150 ikiwa ni thamani ya wachezaji kama kijana Ansu Fati, Memphis Depay pia Real Madrid nao sio wanyonge na namba tatu ipo mikononi mwa Atletico Madrid.

SOMA NA HII  BILIONEA WA LIVERPOOL AJITOKEZA KUTAKA KUINUNUA CHELSEA...MATAJIRI WENGINE HAWA HAPA...

Seria A napo wapo vizuri kwenye mkwanja ambapo Juventus wanatajwa kuwa namba moja kwa kuwa na kikosi na safu ya ushambuliaji ghali na kinatajwa kuwa na thamani ya pauni milioni 618.

Hiki ni kiasi cha chini katika ligi za Ulaya kwa timu ambazo zinaongoza ila AC Milan, Napol, Roma na Inter Milan thamani yao inatajwa kuwa zaidi ya pauni milioni 350.