Home kimataifa JAMES RODRIGUEZ KUIBUKIA AL RAYYAN

JAMES RODRIGUEZ KUIBUKIA AL RAYYAN


BAADA ya kuondolewa kwenye kikosi cha Everton pamoja na kwamba msimu uliopita alionyesha kiwango cha juu, mshambuliaji James Rodriguez anakaribia kutua Qatar.

 

Mshambuliaji huyo mwenye uwezo wa hali ya juu anatarajiwa kujiunga na Al Rayyan ya nchini humo, siku chache baada ya kocha wa Everton, Rafa Benitez kumuambia kuwa hana mpango naye.

 

Winga huyo alijiunga na Everton miezi 12 tu iliyopita akitokea Real Madrid na msimu uliopita alionyesha kiwango cha juu sana uwanjani.

 

Benitez kabla ya kuanza kwa msimu huu alimwambia staa huyo kuwa anatakiwa kutafuta timu ya kwenda kwa kuwa yeye hana mpango naye kwenye timu yake.

 

Kocha huyo wa zamani wa Liverpool alimwambia kwa mpango uliopo kwenye timu yake kwa sasa, Mcolombia huyo hawezi kupata nafasi. Staa huyo mwenye miaka 30, alikuwa akilipwa kitita cha pauni 220,000 kwa wiki akiwa ndiye alikuwa akilipwa zaidi.

 

Rodriguez aliondoka Everton wikiendi iliyopita na anaweza kusaini mkataba mpya na timu hiyo kabla ya wikiendi ijayo akiwa ni mchezaji huru.

SOMA NA HII  MESSI APOTEZWA MAZIMA NA RONALDO