Home Habari za michezo BAADA YA YANGA KUSHINDA JANA…’SURE BOY’ KAONA ISIWE TABU..KAWACHANA HIVI AZAM …

BAADA YA YANGA KUSHINDA JANA…’SURE BOY’ KAONA ISIWE TABU..KAWACHANA HIVI AZAM …


Kiungo Mchezeshaji wa Klabu ya Yanga SC Salum Abubakar ‘Sure Boy” amesema mechi yao ya jana dhidi ya Azam FC ilikua ngumu kutokana na kila timu ilikua inahitaji alama tatu ili kujiweka mazingira mazuri ya msimamo wa ligi kuu ya NBC.

”Ndugu zangu wa Azam FC walikua wamejiandaa ili kuonesha walichokua nacho na haikuwa rahisi wao kuniachia mimi na mimi kuwaachia wao, ila tunamshukuru mungu tumepata alama tatu tunaukaribia ubingwa” alisema Sure Boy.

Sure Boy alicheza jana kwa mara nyingine dhidi ya waajiri wake wa zamani, Azam FC, Ambapo hii inakuwa ni mechi ya pili kukutana toka alipoachana nao mwezi Disemba mwaka jana.

Mechi ya kwanza, kucheza dhidi ya Azam akiwa Yanga ilikuwa mechi ya nusu fainali ya kombe la Mapinduzi, ambapo Azam waliibuka na ushindi kwa mikwaju ya penalti.

Katika mchezo wa jana Yanga walizidi kujiimarisha kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu kwa kuibuka na ushindi wa goli mbili kwa moja.

SOMA NA HII  USAJILI WA NKANE YANGA WAZUA JAMBO...UONGOZI WAGUSIA KUTEMA MCHEZAJI...