Home Habar za Usajili Simba ADEBAYOR AFUNGUKA HAYA MENGINE KUHUSU DILI LAKE NA SIMBA…AWATAJA WAARABU NA KLABU...

ADEBAYOR AFUNGUKA HAYA MENGINE KUHUSU DILI LAKE NA SIMBA…AWATAJA WAARABU NA KLABU YA NORWAY..


STAA wa USGN anayetakiwa na Simba, Victorien Adebayor amesema hakuna mashabiki duniani waliowahi kumfanyia alichofanyiwa juzi usiku timu yake ilipolala mabao 4-0.

Mashabiki wa Simba walimshangaza baada ya kumfuata na kumshangilia kwa nguvu kwenye Basi lao wakati wakiondoka kurudi hotelini. “Sio rahisi mashabiki kuonyesha kitu kama hiki hasa unapokwenda kwao,hii ni upendo mkubwa na heshima kwangu nami nawatakia kila la kheri huko mbele naamini watafanikiwa zaidi,”alisema.

Adebayor alisema ni kweli anazungumza na mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa klabu hiyo Salim Abdallah ‘Try Again’.

Adebayor alisema hata hivyo ofa ya Simba ameiweka mezani akizilinganisha na ofa nyingine nyingi alizonazo huku baadhi zimo klabu za kutoka Afrika Kaskazini ikiwemo RS Berkane na zingine za Morocco na Algeria. “Bado tunazungumza na Rais wa Simba Abdallah (Salim) hatujafikia hatua ya kukubaliana lakini kila kitu kinakwenda vizuri hakuna shida,” alisema Adebayor ambaye kasi yake na ufundi wake wa mguu wa kushoto kila alipogusa mpira mashabiki wa Simba walikuwa wanashtuka.

“Unajua ofa ya Simba ni moja tu kati ya ofa nyingi sana nilizonazo,kuna timu tatu za hili kundi tulilokuwa zinanitaka lakini zipo za Misri na Algeria kwahiyo nitaangalia ipi itakuwa na upekee kwangu mwisho wa msimu.”

Adebayor aliongeza kuwa hata hivyo bado uamuzi wa wapi atakwenda utategemea nani ataweza kumalizana naye yeye pamoja na klabu yake ya nchini Norway ambayo amebakiza mkataba wa miezi 24.

“Bado mimi ni mchezaji halali wa klabu ya HB Køge ya nchini Norway,nimebakiza mkataba wa miaka miwili kwahiyo kuondoka kwangu lazima pia klabu yangu imalizane na klabu ambayo inanitaka nafikiri hili lazima liwe wazi watu waelewe,” aliongeza.

SOMA NA HII  PASI ZA YAO KUAMUA MATOKEO YA YANGA DABI YA KARIAKOO