Home Yanga SC WACHEZAJI YANGA WAPEWA ONYO BAADA YA KAZE KUFUKUZWA

WACHEZAJI YANGA WAPEWA ONYO BAADA YA KAZE KUFUKUZWA


 BAADA ya Klabu ya Yanga kuachana na benchi lao la ufundi lililokuwa likiongozwa na Kocha Mkuu, Cedric Kaze wachezaji nao wamepewa onyo kuacha uzembe ndani ya uwanja katika kusaka matokeo.

Kwa mujibu  wa Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi ndani ya Klabu ya Yanga, Dominick Albinus amesema kuwa baada ya kuachana na Kaze walikaa kikao na wachezaji ili kupeana hesabu za wakati ujao.

“Tumewaambia kwamba wachezaji wetu tayari tumeachana na benchi la ufundi ni kwa sababu yao wenyewe kushindwa kupata matokeo ndani ya uwanja kwenye mechi walizokuwa wakicheza.

“Hivyo kwa kuwaambia hivyo inamaanisha kwamba nao wana kazi ya kuwa makini katika kutimiza majukumu yao kwani kwa sasa timu inahitaji matokeo chanya ndani ya uwanja ili kuweza kufikia mafanikio,” amesema.

Kaze alifutwa kazi rasmi ndani ya Yanga,Machi 7 na mchezo wake wa mwisho ilikuwa mbele ya Polisi Tanzania ambapo alikamilisha kwa sare ya kufungana bao 1-1 baada ya dakika 90. 

Yanga kwenye msimamo ipo nafasi ya kwanza imekusanya jumla ya pointi 50 baada ya kucheza mechi 23, watani zake wa jadi Simba wapo nafasi ya pili na pointi zao ni 45 na wamecheza jumla ya mechi 19.

SOMA NA HII  KUELEKEA MICHUANO YA KLABU BINGWA AFRIKA MSIMU HUU...YANGA WAPANGUA MTEGO WA CAF MAPEMA....KAZI IMEBAKI HAPA...