Home Habari za michezo KIMENUKA SIMBA…DEWJI ATANGAZA KUMTAMBUA MGUNDA KAMA KOCHA MKUU WA TIMU…

KIMENUKA SIMBA…DEWJI ATANGAZA KUMTAMBUA MGUNDA KAMA KOCHA MKUU WA TIMU…

Habari za Simba SC

Wakati wingu zito likizidi kutanda kunako klabu ya Simba SC ikianziwa na hatima yao kunako michezo ya hatua ya Makundi Ligi ya Mabingwa Afrika.

Bado Ubingwa wa Ligi Kuu nao pengo kati yao na vinara Yanga linazidi kuwa kubwa baada ya sare yao na Azam FC juzi na sasa ikiwa ni alama 8.

Kwa matukio hayo mawili makubwa tayari hali ya hewa ndani ya Simba inaonekana kutokuwa shwari kwani wapo mashabiki wanaotaka uongozi ung’oke, lakini kuna wale wanaomnyooshea kidole Kocha Robertinho.

Sasa kubwa kuliko yote ni kauli ya Aliyekuwa mfadhili wa klabu ya Simba, Azim Dewji amesema anamtambua Juma Mgunda kama kocha Mkuu wa klabu hiyo na sio Robertinho.

“Binafsi namtambua Juma Mgunda kama kocha mkuu wa klabu ya Simba, Robertinho ni kama shabiki tu”.

SOMA NA HII  BAADA YA KUANZA KUTUPIA MFULULIZO...FREDY AVUNJA UKIMYA SIMBA...AHMED ALLY ATIA 'UZITO'...