Home Habari za michezo WAKATI HABARI YA MJINI NI ‘MZUNGU’ NA AZIZ KI….KIRAKA WA TZ PRISONS...

WAKATI HABARI YA MJINI NI ‘MZUNGU’ NA AZIZ KI….KIRAKA WA TZ PRISONS KAWATAZAMA WEE…KISHA AKAIBUKA NA HILI…


Ni kawaida ya mashabiki kufanya utani, wakati waliposajiliwa straika wa Simba, Dejan Georgijevic na Stephane Aziz Ki wa Yanga na wakacheza dabi ya Ngao ya Jamii, wapo waliowatania mastaa hao kwamba hawajakutana na kiraka wa Tanzania Prisons, Benjamin Asukile.

Kumbe utani huo Asukile aliuona kupitia mitandao ya kijamii na ukamfanya kuongeze kasi ya mazoezi kuhakikisha anaipa ulinzi wa kutosha timu yake msimu huu.

Alipoulizwa Asukile kama anawafuatilia Ki na Dejan baada ya utani wa mashabiki wa Simba na Yanga? Alijibu; “Nipo tofauti na wachezaji wengine, huwa sifuatilii timu wala mtu yeyote, badala yake nazingatia nidhamu ya kazi na kufanya mazoezi kwa bidii.”

“Unaweza ukamfuatilia mchezaji kumbe kacheza chini ya kiwango ukafanya mazoezi yanayolingana na hilo, kesho akaonyesha uwezo wa juu utafanyaje? Ninamsoma mchezaji ndani ya dakika 10 uwanjani, na kujua uwezo na upungufu wake, kisha najua jinsi ya kufanya jukumu langu.”

Alisema pamoja na kuuona utani huo lakini hajachukulia kama ni chuki, badala yake unauweka kwenye uwejibikaji zaidi.

“Kuna watu walinitumia utani kwamba nyie sajilini huyo Dejan na Ki lakini mjue Asukile na timu yake hawajashuka, nikabaki nacheka tu, maana sijui hata wanafikiria nini, ,” alisema.

Mbali na hilo, Asukile alisema msimu huu timu ina wachezaji wapya kama robo tatu na wameonyesha mwanga wa kuondokana na mateso kama ya ligi iliyoisha.

“Nililowaambia wageni hatutaki kupitia mateso kama tuliyoyapata misimu miwili nyuma, tunahitaji watuongezee nguvu, japokuwa tulichelewa kuingia kambini, ila ninaona wana vitu vikubwa na tukizoeana Prisons hii itakuwa na ushindani mkali,” alisema.

SOMA NA HII  KIBABE SANAAA....MO DEWJI AFANYA KUFRU...AWEKA MEZANI BIL 1 SIMBA WAIFUNGE AL AHLY MISRI..