Home Azam FC MGOLI WA KIBABE WA ‘MZUNGU’ WAIFANYA SIMBA KUWA ‘LEVO’ MOJA NA INTER...

MGOLI WA KIBABE WA ‘MZUNGU’ WAIFANYA SIMBA KUWA ‘LEVO’ MOJA NA INTER MILAN YA ITALIA…ISHU NZIMA IKO HIVI….

Wakati Ligi Kuu Tanzania Bara ikisimama kwa muda katika mzunguko wa pili, vinara kwenye msimamo, Simba imeweka rekodi kama ya Inter Milan kwenye Ligi ya Italia na Villarreal kule Hispania katika mechi za mzunguko huo.

Hiko hivi, kwenye mechi za mzunguko wa pili wa ligi za nchi hizo, Villarreal inayoongoza kwenye msimamo ina pointi na mabao sawa sawa na yale iliyopachika Simba hapa nchini vivyo hivyo kwa Inter Millan kwenye Ligi ya Hispania.

Kwenye mzunguko huo, Simba imekusanya pointi sita ikifunga mabao matano, sawa na matokeo ambayo imepata Villarreal kule Hispania huku Inter Milan yenyewe ikipata matokeo kama hayo, lakini ikiwa imeruhusu bao moja la kufungwa.

Timu nyingine nchini ambazo hazijafungwa wala kutoka sare hadi mzunguko wa pili ni Yanga ambayo ni ya pili kwenye msimamo ikiwa na mabao manne ya kufunga na kufungwa moja na Singida BS ambayo ni ya tatu ikiwa na mabao matatu ya kufunga na moja la kufungwa zote zina pointi sita.

Kule Hispania hadi mzunguko wa pili unafikia tamati, Villarreal ndiyo kinara kwenye msimamo ikiwa na rekodi sawa na ya Simba, ikifuatiwa na Real Madrid, Real Betis na Osasuna ambazo zote hazijafungwa wala kutoka sare zikitofautiana idadi ya mabao.

Madrid imefunga mabao sita na kufungwa mawili, Real Betis imefunga imefunga matano na kufungwa moja na Osasuna imefunga manne na kufungwa moja.

Kwenye Ligi ya Italia, Napoli ndiyo kinara kwenye msimamo ikiwa imepachika mabao 9 na kufungwa mawili, ikivuna pointi sita  sawa na Inter Milan ambayo imefunga mabao matano na kufungwa moja na Roma ambayo imepachika mabao mawili na haijaruhusu nyavu zake kuchanwa hadi mzunguko wa pili.

SOMA NA HII  WAPINZANI WA SIMBA NA YANGA CAF KUJULIKANA WIKI IJAYO...KIMBEMBE KIPO HAPA...