Home Habari za michezo KISA SIMBA…RAIS SAMIA AOMBWA ATOE MIL 200 ZA KUMFUNGA RAJA KWAO….

KISA SIMBA…RAIS SAMIA AOMBWA ATOE MIL 200 ZA KUMFUNGA RAJA KWAO….

Habari za Simba

Kati kati ya wiki Vilabu viwili vinavyoiwakilisha Tanzania katika michuano ya Kimataifa ya Shirikisho la Soka Sfrika (CAF) Simba iliyopo Ligi ya Mabingwa na Yanga waliopo Kombe la Shirikisho viliibuka na ushindi katika mechi zao za hapa nyumbani.

Simba waliitandika Vipers FC kutoka nchini Uganda kwa bao 1-0 na kufufua matumaini ya kusonga hatua ya Robo Fainali, wakalamba milioni Tano za Rais alieahidi kununua kila goli kwa milioni Tano kama sehemu ya kutoa hamasa.

Yanga wakaichapa Real Bamako mabao 2-0 wakabeba milioni zao 10 kwa mabao yao mawili.

Sasa BIKO ARMANDO SCANDA, kupitia Ukurasa wake wa Instagram ametoa ombi kwa Rais kutokana na ahadi hizo za fedha na hamasa kwa vilabu vyetu. Scanda ameandika;

“Mama tumeona hamasa ya milioni tano Kwa goli na tunashukuru sana sababu hela hiyo imewapa nguvu hadi mashabiki. Tupe milioni 200 kabla ya mechi upate heshima ya kunyanyua kikombe cha Afrika msimu huu.

Kwa hali ya waarabu na wakubwa walozoeleka, Mama nakuomba weka Milioni 200 kabla. Nawasilisha kwako Mama @samia_suluhu_hassan. . Kaka yetu @gersonmsigwa tafadhali ujumbe ukufikie, nauona mwanga. Tushirikiane kumtag Mama, Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan. . NB: Mnaiona Simba ina hali mbaya lakini wanaweza kufika Fainali”

SOMA NA HII  SILAHA ZA TAIFA STARS SAFARINI...WAIFATA TIMU NCHINI MISRI