Home Habari za michezo SKUDU AWAPA NENO HILI WANANCHI KUELEKEA MECHI YA SIMBA vs YANGA

SKUDU AWAPA NENO HILI WANANCHI KUELEKEA MECHI YA SIMBA vs YANGA

Habari za Yanga SC

Nyota wa kimataifa wa Klabu ya Yanga, raia wa Afrika Kusini, Skudu Makudubela, amewaahidi Wananchi kuwa watazidi kufurahi kila atakapokuwa anapewa nafasi.

Skudu ametoa kauli hiyo baada ya mchezo uliopita dhidi ya Singida Fountain Gate kuwapa raha Wanayanga kwa muda aliopewa nafasi ya kucheza kipindi cha pili, mchezo ambao ulimalizika kwa Yanga kushinda bao 2-0.

Kuhusu nafasi yake ndani kikosi, Skudu amesema: “Nitaweka juhudi kubwa katika uwanja wa mazoezi ili kumshawishi mwalimu anipe dakika za kutosha. Nawaahidi Wanayanga kuwa watazidi kufurahi kila nitakapokuwa napewa nafasi.”

Mchezo ujao wa Ligi utakuwa kati ya Yanga na Simba, Jumapili ijayo Oktoba 5, 2023 katika Dimba la Mkapa.

SOMA NA HII  MRUNDI WA YANGA APATA OFA TATU MEZANI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here