Home Habari za michezo UZEMBE WA MABEKI SIMBA WAMTIA KIWEWE ROBERTINHO….AANZA KAZI NA CHE MALONE…

UZEMBE WA MABEKI SIMBA WAMTIA KIWEWE ROBERTINHO….AANZA KAZI NA CHE MALONE…

Habari za Simba SC

KOCHA mkuu wa Simba,Roberto Oliviera ‘Robertinho ‘, imetolea uvivu safu ya ulinzi, licha ya kuonekana imara chini ya Che Malone Fondoh na Innonga Baka lakini kwa upande wake bado hajaridhishwa na ufanisi wao kwa kuwepo kwa makosa madogo madogo kila wakati.

Robertinho ametoa kauli hiyo kufuatia na Simba kuruhusu mabao mawili katika Ligi Kuu Bara pamoja na mabao mawili kwenye mechi za kirafiki walizocheza kipindi cha mapumziko ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mchezo wa hatua ya pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Power Dynamo ya Zambia kabla kuwavaa Al Ahly katika michuano ya Supa ligi.

Simba ikiendelea kujifua na mazoezi yao kuelekea mchezo wa hatua ya pili ya ligi ya Mabingwa dhidi ya Power Dynamos utakaopigwa Septemba 16, mwaka huu kwenye uwanja wa Levy Mwanawasa, Zambia na maruadiano yatafanyika Dar es Salaam.

Robertinho alisema anahitaji kuona safu yake ya ulinzi inakuwa makini na kuweza kulinda vyema lango lao kwa kutoruhusu wapinzani kupata nafasi ya kufunga mabao.

Alisema licha ya wachezaji kucheza vizuri bado anaendelea kuwasisitiza mabeki wake wake kuwa makini na kutoruhusu bao kwa wapinzani kama ilivyokuwa kwa michezo minne ambayo wamecheza.

“Safu ya ulinzi bado haijakuwa sawa kwa asilimia 100, unaona jinsi gani tunapata bao lakini wapinzani wanaweza kurudisha, hii ni kutokuwa makini, nimewaeleza mabeki nini cha kufanya.

Naimani kipindi tutakitumia vyema kwa kuweka mambo sawa kwa programu ya mazoezi maalumu kwa mabeki ili kujiweka imara kabla ya kuelekea katika michuano ya kimataifa ambayo inahusisha timu ambazo zinaijua vizuri Simba, ” alisema Robertinho.

Aliongeza kuwa mazoezi yanaendelea vizuri kila mchezaji kutambua majukumu yake, kikubwa kutaka mabeki kuwa makini na kuhakikisha wanaenda kufanya vizuri na kutoruhusu bao kwenye mechi zote mbili dhidi ya Power Dynamos na Al Ahly kuelekea michuano ya AFL.

SOMA NA HII  KUELEKEA DABI LEO....JULIO AFUNGUKA ALIVYOIKOA SIMBA NA AIBU..."NILIMFUKUZA MATOLA"....