UKISEMA wamepania basi wala utakuwa hujakosea hii ni kutokana na kile ambacho kinafanywa na kikosi cha Yanga Princess ambao wamemaliza mzunguko wa kwanza kileleni mwa msimamo na pointi zao 31 huku wakiwa hawajapoteza mchezo wowote.
Yanga inayonolewa na kocha, Edna Lema imekuwa na kasi ya hatari msimu huu ambapo katika michezo 11 waliyocheza wameshinda mechi kumi na kutoa sare mchezo mmoja dhidi ya Simba.
Yanga jana ilimaliza mzunguko wake wa kwanza kwa ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Alliance Girls mabao yaliyofungwa na Tabea Aidano, Emilliana Mdimu, Aniella Uwima na Aisha Masaka aliyeweka kambani mabao mawili.