Home Habari za michezo HUYU NDIYE RAHEEM STERLING….BILIONEA ANAYETESEKA MAN CITY NA KUWINDWA NA CHELSEA…UTAJIRI WAKE...

HUYU NDIYE RAHEEM STERLING….BILIONEA ANAYETESEKA MAN CITY NA KUWINDWA NA CHELSEA…UTAJIRI WAKE WOTE HUU HAPA…


MIONGONI mwa wachezaji ambao wanahusishwa kuhitajika sana na kocha wa Chelsea, Thomas Tuchel ni Raheem Sterling wa Manchester City ambaye huenda akasajiliwa katika viunga hivyo katika dirisha hili.

Sterling ni miongoni mwa wachezaji wanaochukua kiasi kikubwa cha pesa ndani ya EPL na amekuwa akiishi kibosi kutokana na mpunga huo. Cheki hapa jinsi anavyopiga pesa na kuishi kibosi.

ANAPIGAJE PESA

Anapokea mshahara wa Pauni 300,000 kwa wiki ndani ya Man City na ndani ya mwaka anakunja Pauni 15 milioni, utajiri wake kwa ujumla unakadiriwa kufikia dola 66 milioni.

Mshahara huo huongezeka zaidi kutokana na bonasi ambazo anazipata kwa kufunga ama kushinda mechi na kufikia hadi Pauni 320,000 kwa wiki.

Mbali ya mshahara huo Raheem pia anapata pesa kutokana na madili yake mengine nje ya uwanja ikiwa pamoja na lile la Nike alilosaini tangu mwaka 2012.

Pia Anamiliki hisa zenye thamani ya Dola 26.9 milioni kwenye kampuni ya hisa ya Marekani iitwayo Endeavor.

Mbali ya ubalozi wake na Nike fundi huyu pia anaiwakilisha kampuni ya Apple ambayo aliingia nayo makubaliano ya kutangaza bidhaa zao tangu mwaka 2016.

NDINGA

Jamaa kwanza ana gari yake ndogo, yenye thamani ya Pauni 12,000 ambayo aliwahi kuonekana nayo mara kadhaa kwenye mishe mishe zake.

Mbali ya gari hiyo kwenye maegesho ya jamaa pia kuna ndinga nyingine kali kama Range Rovers, Audi S6, Audi Q7, Mercedes C63, Bentley ambazo zote kwa pamoja zinakadiriwa kuwa na thamani ya Dola 4 milioni.

MJENGO

Ana nyumba kali sana moja ikiwa kule Catford, London ambayo inakadiriwa kuwa na thamani ya Dola 2.2 milioni na nyingine ambayo ndio anaishi kwa sasa ni ile iliyopo Jijini Manchester mitaa ya Cheshire ambayo ipo karibu kabisa na ilipo nyumba ya Alex Ferguson. Nyumba hiyo ina thamani ya Pauni 3.5 milioni.

MSAADA KWA JAMII

Amekuwa akijihusisha kwenye kampeni mbali mbali za kupinga unyanyasaji na kusaidia jamii. Miongoni mwa kampeni ambazo aliwahi kushiriki ni pamoja na Kick It Out Football Beyond Borders. Pia anafanya kazi kwa karibu na taasisi ya African-Caribbean Leukaemia Trust ambayo kazi yake kubwa ni kutoa elimu kwa jamii juu ya ugonjwa wa kansa.

SOMA NA HII  PABLO ALIAMSHA HUKO...AKATAA KUPOKEA BARUA YA KUVUNJA MKATABA...ADAI HAKUPANGA KUONDOKA SIMBA MAPEMA...

Juni, 2017 Sterling aliungana wachezaji wengine kwenye kuwachangia pesa wahanga wa tukio la moto la Grenfell Tower ambalo liliondoa maisha ya watu 71.

BATA NA UHUSIANO

Jamaa ana watoto watatu. Kwa sasa yupo kwenye uhusiano wa kimapenzi na mrembo, Paige Milian ambaye amezaa naye watoto wawili huku mtoto mmoja ambaye ni Melody Rose Sterling amezaa na Melissa Clarke. Watoto wawili aliozaa na Milian ni Thiago Sterling na Thai-Cruz Sterling.