Home Habari za michezo HIVI NDIVYO MAYELE ALIMVYOZIDI KUIGARAGAZA SIMBA…AVUNJA REKODI HII NYINGINE KUBWA YA STAA...

HIVI NDIVYO MAYELE ALIMVYOZIDI KUIGARAGAZA SIMBA…AVUNJA REKODI HII NYINGINE KUBWA YA STAA WAO…


Fiston Mayele, mshambuliaji namba moja ndani ya kikosi cha Yanga amevunja rekodi ya staa wa Simba, John Bocco kwenye suala la ufungaji na pasi za mabao.

Bocco msimu wa 2020/21 aliweza kutupia mabao 16 na pasi mbili na aliweza kuibuka mfungaji bora ambaye anatetea kiatu chake hicho.

Msimu huu Bocco kafunga mabao matatu na hajatoa pasi ya bao huku rekodi yake ikivunjwa na Mayele ambaye ametupia mabao 16 na pasi nne za mabao.

Mayele aliifikia rekodi ya Bocco,kwenye mchezo wa ligi uliochezwa dhidi ya Coastal Union ambapo aliweza kufunga mabao mawili na kutoa pasi moja ya bao kwa Chico Ushindi wakati Yanga walipotangazwa kuwa mabingwa wa ligi msimu wa 2021/22.

Mayele amesema kuwa bado anaamini kazi inaendelea katika kutimiza majukumu yake kwenye mechi ambazo zimebaki.

“Bado kuna mechi za kucheza hivyo kazi kubwa ni kuweza kutimiza majukumu yangu nikipata nafasi nitafunga ama kutengeneza nafasi,”.

SOMA NA HII  DAKIKA CHACHE KABLA YA MECHI...AUCHO NA BANGALA WAUNDIWA TUME...