Home Habari za michezo KUHUSU TUZO YA MFUNGAJI BORA BARA…MINZIRO KAFUNGUKA HUYU KUHUSU NAFASI YA MPOLE...

KUHUSU TUZO YA MFUNGAJI BORA BARA…MINZIRO KAFUNGUKA HUYU KUHUSU NAFASI YA MPOLE DHIDI YA MAYELE…


Felix Minziro, Kocha Mkuu wa Geita Gold amesema kuwa bado anaamini kwamba mshambuliaji wake George Mpole ataendelea kutimiza majukumu yake ya kufunga pale anapopata nafasi.

Mpole mpaka sasa ana mabao 16 na pasi tatu za mabao ndani ya ligi sambamba na Fiston Mayele wa Yanga mwenye mabao 16.

Minziro amesema kuwa wachezaji wake wote wapo tayari kwa ajili ya mechi zao na kikubwa ni kupata ushindi.

β€œUgumu wa kupata pointi tatu kwenye mechi tunazocheza ni mkubwa hivyo wachezaji wote ikiwa ni pamoja na mshambuliaji Mpole,(George) bado wana kazi ya kufanya kufunga mabao zaidi.

β€œUnajua ili uweze kupata ushindi ni lazima ufunge kwa maana hiyo hiyo ni kazi ya wachezaji wote na huwa tunafanyia kazi kwenye uwanja wa mazoezi kwa kuwapa mbinu za kufanya wachezaji,” amesema Minziro.

Mpole ana mabao 16 sawa na Mayele akiwa ni mzawa wa kwanza kwa utupiaji ndani ya ligi

SOMA NA HII  SIMBA KUWAFUATA TZ PRISON KWA KASI YA 6G...