Home Uncategorized SIMBA YALAZIMISHA SARE YA KUFUNGANA BAO 1-1 NA WAPINZANI WA YANGA KIMATAIFA

SIMBA YALAZIMISHA SARE YA KUFUNGANA BAO 1-1 NA WAPINZANI WA YANGA KIMATAIFA

BAO la Mshambuliaji wa Simba, Meddie Kagere dakika ya 58 kwenye mchezo wa kirafiki leo dhidi ya Township Rollers lilidumu kwa muda wa dakika 11 pekee.

Township Rollers walisawazisha bao hilo dakika ya 70 kupitia kwa Serameng.

Huu ni mchezo wa tatu kwa Simba kucheza nchini Afrika Kusini kwa ajili ya kujiaandaa na msimu ujao, ambapo ilianza na Orbet TVET ilishinda mabao 4-0 na ilishinda mbele ya Platinum Stars mabao 4-1 kabla ya leo kulamisha sare ya bao 1-1.

Township Rollers itamenyana na Yanga kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa kati ya Agosti 9-11.

SOMA NA HII  AZAM FC YAPANIA KUMALIZA BIASHARA UWANJA WA CHAMAZI JUMLAJUMLA