Home Uncategorized CHAMA ATUA NA UJUMBE WA SHONGA KWA SIMBA

CHAMA ATUA NA UJUMBE WA SHONGA KWA SIMBA

KIUNGO wa Simba Mzambia, Clatous Chama, ametua nchini pamoja na kuanza mazoezi, habari kubwa wanayotaka kusikia Wanamsimbazi ni ujumbe aliyokuja nayo kutoka kwa straika anayezitoa udenda timu zote za Kariakoo, Justin Shonga.

Shonga amekuwa katika midomo ya wapenzi wa Simba tangu msimu uliopita alipohusishwa kusajiliwa na klabu hiyo.

Mchezaji huyo raia wa Zambia anakipiga katika klabu ya Orlando Pirates, lakini ni rafiki wa karibu na Chama ambaye wanacheza pamoja timu ya taifa.

Kitendo cha Chama kuwasili hivi karibuni na jana Mwekezaji na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Simba, Mohammed ‘Mo’ Dewji, kuibuka  na kutoa kauli ya kusema watasajili mchezaji kutoka popote, ni wazi  nyota huyo amekuja na habari njema kuhusu straika huyo.

Shonga amehusishwa kutua Simba kwa mara nyingine tangu usajili wa dirisha dogo msimu huu, lakini bado inadaiwa kuna hali ya mvutano kutokana na dau analohitaji mchezaji huyo.

Inadaiwa Chama ndiye anayetegemewa kumlainisha nyota huyo ili kukubali kutua Msimbazi ukizingatia hana namba ya kudumu katika kikosi cha Orlando.

SOMA NA HII  BABA: HAKUNA STRAIKA WA KUMPITA YONDANI