Home Uncategorized WAKATI WA KUSHUHUDIA KILICHOKOSEKANA KWA MUDA UNAWADIA, MUHIMU KUENDELEA KUCHUA TAHADHARI

WAKATI WA KUSHUHUDIA KILICHOKOSEKANA KWA MUDA UNAWADIA, MUHIMU KUENDELEA KUCHUA TAHADHARI

WAKATI Ligi Kuu Bara ikitarajiwa kuendelea Juni 13 ambapo kutakuwa na mechi mbili ya kwanza itakuwa kati ya Mwadui FC na Yanga na ya pili itakuwa kati ya Coastal Union na Namungo tumeona klabu tayari zimeendelea na maandalizi yake kwa kucheza mechi za kirafiki.

 Mechi za kirafiki zimeweza kuonyesha picha ya kile ambacho wachezaji walikuwa wakikikosa kwa muda mrefu hata hamasa ya mashabiki nayo imeonekana ni kubwa.
   Tangu Machi 17 hakukuwa na mechi yoyote ya ushindani na sababu kubwa ilikuwa ni janga la Virusi vya Corona ambavyo vinaivurugavuruga dunia.
 Kwa kuamua kupambana na janga hilo Serikali iliamua kusimamisha masuala ya michezo ili kuepusha mikusanyiko isiyo ya lazima.
  Baada ya mapambano ya muda mrefu, hatimaye Serikali imeridhia masuala ya michezo kuendelea na iliruhusu masuala hayo kuanza Juni Mosi huku ikisisitiza lazima tahadhari zichukuliwe.
Kwa kuwa wachezaji walikaa nje ya uwanja muda mrefu, benchi la ufundi limeamua kutumia mechi za kirafiki kutambua makosa yalipo ili watakapoanza mechi za ushindani wafanye vizuri.
   Lakini tunaamini kuwa maandalizi ambayo timu zimefanya hakika tutashuhudia  soka safi na lenye ubora   na kupitia michezo hii ya kirafiki  makocha wataangalia ni wapi zaidi wanatakiwa kupafanyia kazi zaidi ilikuleta ushindani na kupata matokeo.
 Pia  urejeo wa ligi hii itatoa picha halisi kwa wachezaji kama kweli walijituma  kwa kuwa fiti au walikuwa  wamebweteka wakati wa mapumziko ya lazima yaliyotokana na janga la Corona.
SOMA NA HII  PACHA YA NCHIMBI NA MOLINGA ILIVYOIBUA MAKUBWA YANGA