Home Habari za michezo KISA WACHEZAJI WA SIMBA KUWA WENGI TAIFA STARS…MANARA AIBUA UPYA VITA YAKE...

KISA WACHEZAJI WA SIMBA KUWA WENGI TAIFA STARS…MANARA AIBUA UPYA VITA YAKE NA BARBARA…AMWITA MSHAMBA…


Baada ya CEO wa Simba SC, Barbara Gonzalez Kuposti kikosi cha Timu ya Taifa na kusindikiza na ujumbe,

“Over one third (36%) of the Tanzania National team is @SimbaSCTanzania” . 9 players out of 25! ➖2 Goalkeepers ➖1 CD ➖1 LB ➖1 RB ➖2 DM ➖2 Strikers

Sasa Msemaji wa Yanga aliyesimamishwa na TFF, Haji Sunday Manara ameibuka na kumshambulia CEO huyo wa Simba akiandika;

Kuna Vitu unapokuwa kiongozi hupaswi kusema,inaleta Ukakasi na ni Ushamba.

Usimba na Uyanga kwenye Timu ya Taifa ni Sumu kubwa kwenye maendeleo ya hii Timu,,tumekuwa tunaleta utimu hadi kwenye National Team na imetugharimu Kwa muda mrefu mno.

Mengine tuwaachie Washabiki Oya Oya wa Mtaani ambao kwao kila kitu ni kutambiana tu,,lakini unapokuwa kiongozi kuna vtu hupaswi hata kuvifikiria.

Last Game Wachezaji wengi waliocheza Taifa Stars,walitoka Yanga na hatukuona kiongozi yoyote wa Club hyo akitamba Kwa hilo,,Coz wanapokuwa pale,wote wanakuwa Wawakilishi wa nchi.

Team yenyewe haipati mashabiki wengi wa kuisapoti Uwanjani ,kisha kiongozi wa Club unaleta ushabiki kisa Wachezaji wa Team yako wengi wamechaguliwa.

Utajisikiaje kuona Mchezaji wa team yako akizomewa uwanjani na shabiki wa Club nyingine? Na Hilo utakuwa hujasababisha ww kwa kuandika ujinga kama huo?

Ni ile Basi tu mengine hatutaki kusema,,katika hao Tisa kuna wengine hata Game moja hawajacheza msimu huu,,inashangaza hata imekuwaje waitwe kwenye hiyo team.

Nb; Je tukubaliane kuwa Tarehe kumi na Tatu iliyofungwa na kina Mayele ni Team ya Taifa?

SOMA NA HII  BAADA YA YANGA KUWAIGA KILA JAMBO....SIMBA WAJA NA HILI JIPYA KUHUSU 'KISPIKA MTAANI'....