Home Habari za michezo MANARA AJIBIZANA NA MWAMAUZI ALIYEWAUA YANGA SAUZI…MWENYEWE AJITETEA NA HILI…

MANARA AJIBIZANA NA MWAMAUZI ALIYEWAUA YANGA SAUZI…MWENYEWE AJITETEA NA HILI…

Habari za Yanga

Kwa mara ya kwanza Mwamuzi wa kati aliyechezesha mechi ya juzi kati ya Mamelodi Sundowns na Yanga Beida Dahane raia wa Mauritania amefunguka kwamba asilaumiwe kwa lolote lile kwenye sakata la goli la Aziz Ki kukataliwa bali lawama zote ziwaendee waliokuwa wana-control Video Assistant Referee (VAR)

Mwamuzi huyo ameeleza hayo wakati aki-chat Instagram na Semaji la Dunia Haji Sunday Manara.

Mwamuzi Beida Dahane ameweka wazi kuwa wakati wa faulo ya @lomalisa4 wanao-control VAR walishindwa kutoa maamuzi hivyo walihitaji msaada wake ndio maana alienda kuwasaidia lakini Kwenye Goli la aziz.ki.10 hakwenda kuthibitisha kwenye VAR kwa sababu haikuwa kazi ngumu kwa wanao-control VAR kutoa maamuzi, walimueleza mapema kuwa sio goli, hivyo kama kuna makosa yoyote walaumiwe wao.

Mwamuzi Beida Dahane @dahane_23 amefunguka kuwa hawezi kuomba msamaha kwa Watanzania kwani hakuhusika katika maamuzi, kama kuna kosa lolote amefanya basi ataomba msamaha kwa Mungu.

Mwamuzi Beida Dahane amesisitiza kwamba yeye ndiyo anatakiwa kuombwa msamaha maana anashambuliwa sana kutokana na sakata hili, wakati wanaotakiwa kushambuliwa ni watu wa VAR.

SOMA NA HII  JAMES KOTEI 'MIWILI TENA'....SINGIDA BIG STARS 'WAMPIGA OFA' NONO YA 'KUFA MTU'...MWENYEWE AKUNJUA ROHO KILAINIII...

3 COMMENTS

  1. Lawama ni lazima azibebe mwamuzi wa Kati. Kama si Goal basi Yanga walistahili kupiga mpira wa kona. Lakini referee hata hilo hakuliona.

  2. Kama anasema asilaumiwe maana yake ni kwamba anakubali kuna tatizo katika kile walichofanya ila tu anasema yeye siyo chanzo. Watafiti wa michezo ya Bahati Nasibu kwenye kipindi cha BBC news waliisha wahi kusema kuwa kuingiza betting kwenye soka ni kosa. Itaua maudhui yaliyopelekea kuanzisha kwa huu mchezo. Moja ya sababu ilikuwa ni kupunguza uhasama uliokuwepo kwenye jamii nyakati hizo, kwa staili hii FIFA wanaturudisha kulekule.

  3. It needs a madman to agree on what the referee is saying . Weak defence if at all he is defending himself.
    Corruption in football will destroy the flavour of the game