Home Habar za Usajili Simba ACHANA NA HABARI ZA UTAMBULISHO WA OUATTARA….HAYA HAPA YA UMUHIMU UNAFAA KUYAJUA...

ACHANA NA HABARI ZA UTAMBULISHO WA OUATTARA….HAYA HAPA YA UMUHIMU UNAFAA KUYAJUA KUHUSU USAJILI WAKE…


Klabu ya Simba imemtambulisha beki wa kati, Mohammed Ouattara kutoka Klabu ya Al Hilal ya Sudan.

Mchezaji huyo (29), raia wa Bukina Faso ni miongoni mwa chaguo la Kocha Zoran Maki ambaye wamewahi kufanya kazi pamoja nchini Sudan katika Klabu ya Al Hilal.

Ouattara amesaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia Simba ambayo awali  ilikuwa kwenye rada za kumnasa beki wa St George ya Ethiopia, Mghana Edwin Frimpong, lakini Kocha Zoran Maki alivyotua akapendekeza usajili wa Ouattara ambaye anamfahamu zaidi.

Beki huyo ndiye mbadara wa Pascal Wawa ambaye mkataba wake ulifikia tamati mwishoni mwa msimu uliopita.

Usajili wa Ouattara unaifanya  Simba kuwa na mabeki wa kati wanne ambao nini Joash Onyango, Inonga Baka, Erasto nyoni na Kenedy Wilson.

Ouattara ni mchezaji wa sita mpya kutambulishwa Simba msimu huu wa dirisha kubwa, wengine ni Moses Phiri, Habib Kyombo, Augustine Okrah, Victor Akpan na Nassor Kapama.

Simba kwa sasa imeweka kambi huko Ismailia, Misri kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania bara na Ligi ya Mabingwa Afrika.

SOMA NA HII  BAADA YA KUSHINDWA KUWIKA MSIMU HUU...CHAMA AWAANGUA SIMBA...UJUMBE WAKE HUU HAPA...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here