Home Habari za michezo MASHABIKI WA SIMBA ..ALICHOKIONGEA CHAMA HUKO MISRI MMEKISIKIA KWELI…AMEUNGUKA A-Z KUHUSU MALALAMIKO...

MASHABIKI WA SIMBA ..ALICHOKIONGEA CHAMA HUKO MISRI MMEKISIKIA KWELI…AMEUNGUKA A-Z KUHUSU MALALAMIKO YENU..


Kiungo fundi wa Simba, Clatous Chama amesema msimu ujao analenga kupambana zaidi ili kuisaidia timu kushinda kila mechi kufikia mafanikio waliyojipangia.

Chama alisema wakati anaondoka Simba kwenda RS Berkane msimu uliopita kabla ya kurejea alikuwa kwenye kiwango bora tofauti na miezi sita aliyotumikia timu baada ya kurejea.

Alisema miongoni mwa sababu zilizokuwa changamoto kwake ni majeraha yaliyomsumbua muda mrefu hadi kushindwa kucheza mechi nyingi, ila sasa hivi yupo fiti na tayari kuipigania timu.

“Unajua watu wengi wananiulizia na hadi wengine kulalamika wanaamini nipo kwenye kiwango bora na naweza kufanya jambo kwa ajili ya timu na hilo ndilo nimeliweka moyoni nataka kulifanya kwenye mechi za msimu ujao,” alisema Chama.

“Niliweka rekodi mbalimbali huko nyuma zote zilikwenda kuinufaisha timu na sio Chama binafsi hilo ndilo nimeliweka moyoni mwangu na nataka kwenda kulifanya wakati huu.

“Ukiangalia misimu minne iliyopita tulitengeneza ukubwa wa klabu na haukuja tu, bali ulitokana na kufanya vizuri kwetu mashindano ya ndani, kimataifa na hilo tunataka kulifanya tena msimu ujao kulingana na timu ilivyo naamini linawezekana.”

Chama alisema kambi yao Misri ina ushindani mkubwa kila mchezaji akitaka kuonyesha uwezo kila zoezi ambalo benchi la ufundi linawapatia.

SOMA NA HII  ISHU YA UCHAGUZI TFF, MAHAKAMA YATOA MAAMUZI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here