Home Habari za michezo KISA TUHUMA ZA USHIRIKINA…MBRAZILI AINGILIA KATI BIFU LA KAPOMBE NA MWENDA…ISHU NZIMA...

KISA TUHUMA ZA USHIRIKINA…MBRAZILI AINGILIA KATI BIFU LA KAPOMBE NA MWENDA…ISHU NZIMA IKO HIVI…

Habari za Simba

Benchi la ufundi Simba chini ya Kocha Robertinho limekata mzizi wa fitina kwa kumaliza bifu linalodaiwa kuwapo baina ya mabeki wa kulia, Shomary Kapombe na Israel Mwenda baada ya kuwaweka chini na sasa kila kitu kinaenda sawa.

Awali inaelezwa mabeki hao walikuwa hawaivi, kiasi cha Mwenda kudaiwa kugoma kujiunga na timu licha ya kupona majeraha yake, japo mabosi wa klabu hiyo walikuwa wakificha, ila habari za ndani zinasema kazi kubwa iliyofanywa na Mbrazili kumaliza bifu hilo.

β€œRobertinho na jopo lake waliwaweka chini na kurekebisha mambo na kila kitu sasa kipo sawa ndio maana umeona Mwenda kajiunga na timu na ameungana na wenzake kwenye msafara baada ya kukosekana kwa muda mrefu,” kilisema chanzo makini.

Hivi karibuni kulizuka sintofahamu kati ya mabeki hao wawili wa Simba , ambapo taarifa kutoka kwa watu wao wa karibu zilidai kuwa wachezaji hao wa Taifa Stars wamekuwa wkitupiana maneno kuhusu mambo ya kishirkina.

Katika kukoleza madai hayo, Shomary kapombe katika moja ya mahojiano na chombo kimoja cha habari alikiri kuwa toka siku za hivi karibuni amekuwa akiugua magojwa ambayo hata madaktari wanashindwa kutambua.

Hata hivyo, wakati Mwenda naye alipokuwa majeruhi alitupa dongo gizani akidai kuwa kuna mambo ya giza amekuwa akifanyiwa japo wote hawakubainisha muhusika ni nani.

SOMA NA HII  KOMBE LA YANGA DAR..:MANARA NA SENZO WASHUKA KLABU YA SIMBA NA KOMBE...MASHABIKI WAWACHANGAMKIA CHAP...