Home news WANAIJERIA WAIPA MBINU SIMBA KUIMALIZA YANGA KWA MKAPA

WANAIJERIA WAIPA MBINU SIMBA KUIMALIZA YANGA KWA MKAPA


 MABOSI wa Simba wameweka wazi kuwa imani kubwa kwenye mchezo wao wa leo dhidi ya Yanga ni kubwa kutokana na mbinu ambazo wamezinasa kitaalamu kupitia mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Rivers United.

Taarifa kutoka Simba zimeeleza kuwa benchi la ufundi la Simba halikuacha kuwafuatilia wapinzani wao kwenye mechi zao mbili za kimataifa dhidi ya Rivers United jambo ambalo linawapa nguvu ya kushinda mchezo wao.

“Yanga ni timu nzuri hivyo kuifuatilia pia inahitaji mbinu nzuri zitakazosaidia kupata ushindi, mechi zao mbili za kimataifa zinatoa picha kamili kwa sababu huwezi kuficha mbinu ya kusaka ushindi kwenye mechi kubwa, kuzitazama mechi zile kunamaana kubwa kwetu,” ilieleza taarifa hiyo.

Alipotafutwa Kaimu Ofisa Habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga aliliambia Championi Jumamosi kuwa maandalizi yapo vizuri na kuhusu kuwafuatilia wapinzani wao hilo ni jukumu la benchi la ufundi.

“Kuangalia mpinzani wako nini anafanya hilo lipo kwenye benchi la ufundi ila tunajua kwamba Yanga ilikuwa inawakilisha Tanzania kwenye Ligi ya Mabingwa. Wachezaji wetu wapo tayari na imani yetu ni kuona kwamba tunafanya vizuri,” alisema Kamwaga. 

Simba ni mabingwa watetezi wa Ngao ya Jamii waliitwaa msimu uliopita walipomenyana na Namungo FC na iliibuka na ushindi wa mabao 2-0.

Ni nyota wawili ambao watakosekana waliotwaa pamoja Ngao ya Jamii msimu uliopita ni Clatous Chama na Luis Miquissone ambao wameuzwa mazima.

SOMA NA HII  KISA SIMBA...BANGALA AENDA KWAO CONGO 'KUJIBUSTI'..NADI AKUNA KICHWA..AFUNGUKA HAYA...