Home Uncategorized ASTON VILLA WAPATWA NA BAMFORD, WACHAPWA

ASTON VILLA WAPATWA NA BAMFORD, WACHAPWA



ASTON Villa wakiwa nyumbani hawatamsahau mshambuliaji wa Klabu ya Leeds United, Patrick Bamford kwa kuwatungua hat-trick kwenye mchezo wa Ligi Kuu England wakati wakipoteza kwa kufungwa mabao 3-0.

Kujiamini na uwezo wa Bamford uliiponza timu ya Aston Villa ambayo Mtanzania Mbwana Samatta aliweka rekodi ya kucheza hapo msimu uliopita kabla ya kutolewa kwa mkopo kuelekea nchini Uturuki.

Mabao ya mshambuliaji huyo mwenye miaka 27 yalipachikwa dakika ya 55, 67 na 74 na kuwafanya Leeds kusepa na pointi tatu mazima Uwanja wa Villa Park na kuwafanya Villa wapoteze mchezo wao wa kwanza kwa msimu wa 2020/21 kwa kuwa walikuwa wamecheza mechi nne bila kupoteza.

Matokeo hayo yanaifanya Aston Villa kuwa nafasi ya pili na pointi zake 12 huku Leeds ikiwa nafasi ya tatu na pointi 10 baada ya kucheza mechi sita ndani ya Ligi Kuu England ambayo imeanza kwa kasi kubwa msimu huu na kinara ni Everton mwenye pointi 13.

SOMA NA HII  ANAANDIKA HAJI MANARA KUHUSU JONAS MKUDE