Home Habari za michezo KUTOKA TUNISIA…YANGA ‘WAJIWEKA MGUU SAWA’…KAZE AVUNJA UKIMYA HALI ILIVYO…

KUTOKA TUNISIA…YANGA ‘WAJIWEKA MGUU SAWA’…KAZE AVUNJA UKIMYA HALI ILIVYO…

Habari za Yanga

Kikosi cha Yanga kimefanya mazoezi ya kwanza ya ufundi asubuhi ya jana kwenye viwanja vya Olympic de Rades nchini Tunis, Tunisia kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya US Monastir ya nchini humo.

Mazoezi haya yaliodumu kwa saa moja na nusu yalianza saa 10:30 kwa saa za Tunisia [Sawa na saa 12:30 mchana kwa Tanzania].

Akizungumza na Yanga Media kocha msaidizi wa Yanga, Cedric Kaze alisema, wao kama benchi la ufundi wanafurahishwa na maandalizi mazuri yaliyofanywa na uongozi wa Yanga kuelekea mchezo wa Jumapili, dhidi ya Monastir ya Tunisia.

“Leo (jana) tumefanya mazoezi ya pili hapa Tunisia, jana tulianza na recovery na leo tumekuja uwanjani. Kila kitu mpaka sasa kiko sawa na wachezaji wanaonyesha kuwa na furaha na kujituma sana,” alisema Kaze.

Wachezaji wote 24 walihudhuria mazoezi haya yaliyosimamiwa na kocha mkuu, Nasredine Nabi kasoro golikipa Aboutwaleb Mshery aliyesafiri kwenda Sousse kwa ajili ya matibabu.

SOMA NA HII  SAKATA LA MWAKINYO KUPIGWA UINGEREZA...MANDONGA NAYE KAONA ISIWE TABU...AIBUKA NA KUMSHUKIA KWA MANENO HAYA..