Home Yanga SC INJINIA HESRSI: SIO KISINDA TU, HATA YACOUBA, MUKOKO NAO WANA OFA

INJINIA HESRSI: SIO KISINDA TU, HATA YACOUBA, MUKOKO NAO WANA OFA


UONGOZI wa Yanga umebainisha kwamba sio Tuisila Kisinda ambaye amepewa ofa bali wapo wengine wengi ndani ya kikosi hicho ambao wamepewa ofa kwa ajili ya kujiunga na timu nyingine.


Injinia Hersi Said, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ndani ya Yanga amesema kuwa suala la kuuza wachezaji wenye hadhi kwa Yanga limekuwa likifanyika.

Hersi ameweka wazi kwamba hilo linatokana na uwezo wa wachezaji ambao wapo ndani ya timu hiyo.
“Suala la kuuza wachezaji limefanyika sana kwa hiyo ofa zipo za wachezaji sio Kisinda tu zipo ofa nyingi kwa wachezaji.

“Kuna ofa ya Yacouba, (Songne), Tonombe, (Mukoko) hivyo ambacho kinaangaliwa ni namna ya kuweza kufanya biashara pamoja na kupata mbadala wake,” amesema.
SOMA NA HII  GAMONDI APATA WASIWASI, PACOME, MAXI WAZUO HOFU, ISHU IKO HIVI