Home Habari za michezo UANAAMBIWA KWA HAYA ANAYOPITIA MAYELE HUKO YANGA…MPAKA KAZE MWENYEWE ANASHANGAA…

UANAAMBIWA KWA HAYA ANAYOPITIA MAYELE HUKO YANGA…MPAKA KAZE MWENYEWE ANASHANGAA…


KOCHA Msaidizi wa Yanga, Cedrick Kaze amesema anashangazwa na mashabiki wa soka wanaombeza straika wa timu hiyo, Fiston Mayele baada ya kushindwa kutetema katika mechi mbili mfululizo zilizopita huku akikiri, kwake ndiye mchezaji bora wa msimu.

Mayele hajafunga katika mechi dhidi ya Simba na Ruvu Shooting kitendo kilichofanya baadhi ya mashabiki na hata wadau wa soka kumbeza na kudai ni mchezaji wa kawaida anayezifunga timu ndogo na dhaifu, kitu kilichomshtua Kaze na kusema hawamtendei haki straika huyo kwani amehusika kwa asilimia 60 ya mafanikio iliyonayo Yanga sasa.

Kaze, alisema soka ni mchezo wa wazi kila mmoja ana jicho lake, ila kwake kabla hata ya msimu haujamalizika anaona kabisa Mayele anastahili kuwa Mchezaji Bora wa msimu na kwa Yanga pia.

“Unambeza mchezaji ambaye kwa asilimia kubwa amehusika kuifanya Yanga ifike ilipo sasa, amefunga ametoa pasi za mwisho kwa wenzake, si mchezaji wa kusubiri kutengewa mipira ni mpambanaji anakupa vitu vingi uwanjani atakaba na atashambulia anakuwaje abezwe eti wa kawaida?” Alihoji Kaze na kuongeza:

“Mayele hakusajiliwa ili afunge tu, ingekuwa hivyo angekuwa anasubiri alishwe mipira, lakini jamaa akakupa kitu muhimu na bora uwanjani hivi vyote vinatakiwa kuangaliwa kabla ya kumkosoa.”

Mayele aliyesajiliwa msimu huu akitokea AS Vita ya DR Congo amefunga mabao 12 na kuasisti mara tatu akilingana na George Mpole wa Gieta Gold, akiifanya Yanga iwe kileleni kwa muda mrefu na pointi 56 baada ya mechi 22, ikishikilia rekodi ya kuwa timu pekee isiyopoteza hadi sasa katika Ligi Kuu.

SOMA NA HII  NYOTA HAWA WATATU WA YANGA KUIKOSA RIVERS UNITED

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here