Home Habari za michezo NOVATUS ANUKIA LIGI KUU UINGEREZA….MPANGO MZIMA UNASUKWA HIVI…

NOVATUS ANUKIA LIGI KUU UINGEREZA….MPANGO MZIMA UNASUKWA HIVI…

Habari za Michezo

NI SUALA la muda tu, ndivyo anavyoamini Geofrey Elias maarufu kama Jeff Megan kuwa mchezaji kinda wa Kitanzania, Novatus Dismas miaka michache ijayo anaweza kucheza soka la kulipwa Ligi Kuu England.

Megan anayeishi Ubelgiji amesema kinachompa ujasiri wa kusema hilo ni vile makocha na wachezaji wanavyomzungumzia Novatus ambaye kwa sasa anaichezea FC Shakhtar Donetsk ya Ukraine.

Ukaribu wa Megan na wachezaji wa Kitanzania ambao wanacheza soka la kulipwa Ulaya, umemfanya kupata nafasi ya kuongea na makocha mbalimbali wakubwa akiwemo Mbaye Leye ambaye aliinoa S.V. Zulte Waregem msimu uliopita kabla ya kibarua chake kuota nyasi.

“Uzuri wa Novatus ni mchezaji mwenye uwezo wa kucheza nafasi zaidi ya mbili uwanjani tena kwenye kiwango kizuri tu na namna ambavyo mwalimu amekuwa akitaka, nakumbuka Leye aliwahi kusema anaweza kufika mbali kutokana na umri wake bado mdogo,” alisema Megan.

Megan alikuwa karibu na Novatus wakati akicheza soka la kulipwa Ubelgiji na hata baada ya mchezaji huyo kwenda Ukraine ameendelea kuwa anamtembelea na kutazama mechi ambazo amekuwa akicheza.

Miongoni mwa ndoto alizonazo Novatus ni kucheza Ligi Kuu England ambayo amekuwa akiifuatia tangu akiwa mdogo na mara kadhaa amekuwa akiliweka wazi hivyo kuichezea Shakhtar anaamini ni hatua ya kupigania hilo.

SOMA NA HII  PLANI ZA SIMBA KWA KMC KESHO HIZI HAPA...MGUNDA NI KAMA KAMALIZA KAZI HIVI...