Home Uncategorized SAID NDEMLA MAMBO BADO NDANI YA SIMBA

SAID NDEMLA MAMBO BADO NDANI YA SIMBA

SAID Ndemla, kiungo wa Simba i

naonekana amewagawa viongozi wa timu hiyo ambapo wapo wale wanaotaka nyota huyo aongezewe kandarasi na wengine wanataka asiongezewe.

Habari zinaeleza kuwa nyota huyo amepewa mkataba wa awali ili aupitie kabla ya kusaini dili jipya kuendelea kukipiga ndani ya Simba iliyo chini ya Bilionea Mohammed Dewji,’Mo’.

Pia kiungo huyo alihusishwa kuibukia Yanga msimu ujao mkataba wake utakapomeguka ila bado maamuzi ya kumuongezea mkataba hayajapitishwa.

“Bado Ndemla anajadiliwa kuhusu kumuongezea mkataba wake wa kuendelea kukipiga Simba hiyo ni baada ya kocha kuonekana hana mipango naye katika kikosi chake hivyo viongozi wanaendelea kumjadili kama wakikubaliana kwa pamoja kumpitisha basi ataongezewa mkataba,” ilieleza taarifa hiyo.

Katibu Mkuu wa Simba, Arnold Kshembe amesema:” Muda wa usajili bado haujafikia hivi sasa viongozi akili zetu tumezielekeza kwenye ubingwa wa ligi tu, baadaye tunaweza kuwa na nafasi ya kulizungumzia hilo.”

SOMA NA HII  YANGA WAPEWA BURE MBADALA WA MAKAMBO