Home news KIMEUMANAAH..SERIKALI WATOA TAMKO SAKATA LA GSM KUDHAMINI TIMU NYINGI LIGI KUU…TFF WAPEWA...

KIMEUMANAAH..SERIKALI WATOA TAMKO SAKATA LA GSM KUDHAMINI TIMU NYINGI LIGI KUU…TFF WAPEWA AGIZO..

 


Serikali hatimaye imetoa msimamo wake kuhusu kampuni ya GSM kudhamini timu zaidi ya moja na kueleza kuwa hilo wanawaachia Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa kuwa ndio inaangalia sheria.

Hatua hiyo inakuja baada ya hivi karibuni GSM kutangaza kuzidhamini timu za Pamba na Coastal Unioni ya Jijini Tanga, ukiachilia mbali kuwa bado wanawadhamini Yanga SC.

Kutokana na hilo wadau mbalimbali wa mpira wa miguu wamekuwa na mtazamo tofauti huku wengine wakihofia huenda GSM ikaingilia katika kupanga matokeo.

Hata hivyo  jana Jumamosi Novemba 6, 2021, gazeti la Mwanaspoti walitaka kusikia kwa upande wa serikali inalizungumziaje suala hilo na akitolea ufafanuzi Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Innocent Bashungwa, amesema hawaoni kama lina shida endapo sheria zitafuatwa.

 “Ukiachilia mbali TFF pia tuna baraza la Michezo (BMT) ambalo lipo karibu katika kusimamia sheria hizo, hivyo sioni na wala wananchi wasiwe na shaka katika hilo  kwani kama kutatokea ukiukwaji wowote hawatasita kuchukua hatua kwa muhusika” amesema Waziri huyo.

Pia Bashungwa amesema katika suala hilo la udhamini wa GSM watu wasitie shaka nalo kwa kuwa kama ni sheria za mpira zipo, hivyo endapo kutaonekana kuwa na mambo tofauti wahusika

SOMA NA HII  ARSENAL YA ARTETA NA MBIO ZA UBINGWA EPL.....MAN CITY, LIVER WATABAKI SALAMA?