Home Uncategorized KOCHA MANCHESTER UNITED YADAIWA CHANZO LUKAKU KUSEPA

KOCHA MANCHESTER UNITED YADAIWA CHANZO LUKAKU KUSEPA


IMEELEZWA kuwa Romelu Lukaku hakuwa na amani ndani ya kikosi cha Manchester United kutokana na kutibuana na Kocha Msaidizi wa timu hiyo kabla ya kutimkkia zake Inter Milan.

Mike Phelan ambaye ni Kocha Msaidizi wa United alizinguana na Lukaku walipokuwa kwenye maandalizi ya msimu mpya.

Sababu kubwa ya mgogoro huo ni kuchelewa ndani ya basi walipokuwa mashariki ya mbali.

Ishu inaelezwa kuwa Lukaku alipaswa awahi ndani ya basi kwa ajili ya ukaguzi pamoja na kusepa na wenzake walipokuwa hotelini Shanghai ila akachelewa.

Meneja Mkuu, Ole Gunnar Solskjaer alipewa taarifa, ila Phelan akamwamuru dereva kuondoa gari na ikwa hivyo jambo lililomfanya Lukaku aende uwanjani mwenyewe maana hakuwa na namna alipomweleza Phelan picha likaanzia hapo wakaanza kutupiana maneno.

SOMA NA HII  BEKI TANZANIA PRISONS: TUNAKOSA UHURU KWA SASA