Home Taifa Stars NDAYIRAGIJE MATUMAINI KAMA YOTE MBELE YA CHIPOLOPOLO

NDAYIRAGIJE MATUMAINI KAMA YOTE MBELE YA CHIPOLOPOLO


KOCHA mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Etienne Ndayiragije amesema kuwa ana matumaini makubwa kwamba kikosi chake kitaanza vizuri kampeni ya michezo ya CHAN inayofanyika nchini Cameroon kwa kuifunga timu ya Taifa ya Zambia ‘Chipolopolo’.

Stars tayari imetua nchini Cameroon na kikosi cha wachezaji 27 kwa ajili ya michuano hiyo huku mchezaji wa klabu ya Simba, Erasto Nyoni na kocha Seleman Matola wakiwa njiani kujiunga na kikosi hicho baada ya kumaliza majukumu yalikuwa yakiwakabili.

Kikosi cha Stars kimepiga kambi katika Jiji la Limbe kikiendelea na mazoezi katika uwanja wa Centenary, kujiandaa na mchezo wa kwanza wa kundi D dhidi ya Zambia utakaopigwa kesho kutwa Jumanne, kabla ya kucheza mchezo wa pili dhidi ya Namibia Januari 23 na kumalizia na Guinea Januari 27.

Akizungumzia kuhusu maandalizi yao, Ndayiragije amesema: “Tunashukuru kwa kuwasili salama nchini Cameroon kwa ajili ya michuano hii ya CHAN ambapo tayari tumeanza mazoezi ya kujiandaa na michezo yetu ya kundi D, hasa ule wa ufunguzi dhidi ya Zambia ambao ni muhimu zaidi tukashinda ili kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kushinda michezo yetu inayofuata,”

SOMA NA HII  BREAKING;KIM POULSEN, KOCHA MKUU WA TAIFA STARS