Home Uncategorized ALIYEWAPIGA HAT TRICK SINGIDA UNITED ATAJA KINACHOMBEBA

ALIYEWAPIGA HAT TRICK SINGIDA UNITED ATAJA KINACHOMBEBA


KELVIN Sabato, nyota anayekipiga ndani ya kikosi cha Kagera Sugar amesema kuwa katika maisha yake ya soka amekuwa ni muumini mkubwa wa kujituma ndani ya uwanja jambo ambalo linamfanya awe bora.

Kabla ya Ligi Kuu Bara kusimamishwa Sabato alikuwa ametupia mabao sita huku akiwa na mpira mmoja kabatini mwake baada ya kuitungua hat trick Singida United.

Sabato amesema:”Kikubwa ni kuwa muumini mzuri wa kujituma ndani ya uwanja na kufanya juhudi pale ninapopata nafasi jambo ambalo lilinibeba.

“Kwa sasa wakati huu wa maambukizi ya Virusi vya Corona ni kwamba mambo sio shwari kwani mipango mingi imeyumba, ila mwishio wa siku kila mmoja ni lazima achukue tahadhari ili kuwa salama,” amesema.

Sabato aliibukia Kagera Sugar akitkea klabu ya Gwambina inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza ambayo iliinasa saini yake kutoka Mtibwa Sugar.

SOMA NA HII  PSG BADO WANAIMANI YA KUMPATA MESSI